Jumamosi 18 Aprili 2026 - 17:30
Ikiwa tutasuasua katika usimamizi wa Mlango wa Hormuz, wengine wataingia/ Diplomasia ya kujibu tu imekatazwa

Hawza/ Imamu wa Ijumaa wa Qom, huku akibainisha kuwa; Iran inapaswa kuchukua hatua ya awali katika Mlango wa Hormuz na kutoka katika hali ya kujibu tu kwenda katika hali ya kuwa mbunifu, mtunga kanuni na mdai, alisema: Haipaswi Mlango wa Hormuz kubakia katika kiwango cha kukusanya tozo na kupata mapato ya muda mfupi tu; bali ni mojawapo ya sifa za kimkakati za Iran na chombo cha utawala katika anga ya kimataifa ambacho huathiri mahusiano ya kimataifa, mipangilio ya kiusalama na lugha ya mazungumzo na nchi nyingine.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Sayyid Muhammad Saeedi katika khutba za Ijumaa za wiki hii mjini Qom zilizofanyika katika Msikiti wa Muswalla Quds, huku akifasiri Aya ya 18 ya Suratul-Fath tukufu, inayojulikana kama Aya ya Ridhwan, alisema: Aya hii ni miongoni mwa vipengele muhimu vinavyoelezea uhusiano baina ya kiongozi (waliyy) na umma.

Imamu wa Ijumaa wa Qom aliendelea kusema: Kutoa bai‘a kwa waliyy kwa mtazamo wa Qur’ani si mkataba wa kisiasa na kijamii tu; bali ni jukumu la kidini na sababu ya radhi za Mwenyezi Mungu, na matokeo yake ni utulivu wa nyoyo za Waumini katika misukosuko na migogoro mikali ya jamii. Jamii iliyochini ya Walii al-Amr haipatwi na hofu wala kusambaratika, na malipo ya kudumu juu ya bai‘a hii ni ushindi na kufunguliwa (fat-h).

Khatibu wa Ijumaa wa Qom alitaja bai‘a ya Ridhwan kuwa ni bai‘a ngumu ambayo Waumini walijua kuwa kujifunga nayo kwa vitendo huenda kukagharimu maisha yao, na akasema: Mwenyezi Mungu Mtukufu alipouona ukweli wa Waumini hawa katika bai‘a yao, alibadilisha hali kwa manufaa ya wale waliotoa bai‘a.

Mfanano wa bai‘a ya watu kwa Imamu wa tatu wa Mapinduzi na bai‘a ya Ridhwan kwa Mtume (saww)

Akiilinganisha Aya ya 18 ya Suratul-Fath na hali ya leo nchini Iran, alisema: Kama vile bai‘a ya Ridhwan ilivyofanyika katika kilele cha vitisho vya adui, ndivyo pia bai‘a ya watu wetu kwa Hadhrat Ayatullah Imam Sayyid Mujtaba Husseini Khamenei ilivyofanyika katika nyakati hatari na nyeti; kiasi kwamba nchi ilikuwa ikikabiliwa na changamoto kubwa na vitisho vya nje, na uwepo huu wa watu na bai‘a yao unaonesha uimara wa muundo wa ndani wa nguvu katika Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Trump mhalifu baada ya kuuawa kishahidi Imamu wa Umma alitangaza kuwa kiongozi ajaye wa Iran nitamchagua mimi, lakini taifa letu kwa ngumi zilizokunjwa lilimpiga mdomoni na kusema: unafanya kosa kubwa.

Ayatullah Saeedi alielezea mfanano wa pili kati ya bai‘a ya watu wetu na bai‘a ya zama za Mtume kuwa ni mwendelezo wa njia ya wilaya, na akasema: Lengo na njia ni moja, na muendelezo huu unaonesha kuwa bendera ya wilaya haitowahi kuanguka chini katika zama zozote; kama alivyosema Imaam Ali (as), kuhusu ubebaji huu wa bendera: bendera hii haibebwi isipokuwa na mwenye basira na subira.

Aliongeza: Mfanano wa tatu wa bai‘a ya leo na bai‘a ya Ridhwan umejengwa juu ya vipengele viwili: ikhlasi na ushindi wa karibu; ikiwa bai‘a hii itakuwa kwa ukweli wa moyo, malipo yake ni ushindi wa karibu. Umoja wa taifa na uongozi unaweza kusababisha ustawi katika safu ya mapambano na kuvuka migogoro, na uhusiano kati ya umma na Walii al-Amr ndio siri ya kuvuka kutoka katika hofu kwenda kwenye usalama, na kutoka kwenye tishio kuelekea katika ushindi.

Siku ya Msichana iliyo tofauti

Imamu wa Ijumaa wa Qom katika khutba ya pili, akibainisha kuwa Jumapili ijayo ni siku ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Hadhrat Ma‘suma (as), Siku ya Msichana, na mwanzo wa muongo wa Karama, alisema: Muongo wa Karama mwaka huu si tu kuadhimisha kuzaliwa kwa Ahlul-Bayt (as); bali kwa kuuawa kishahidi Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, wanafunzi wa shule ya Shajarat Tayyiba ya Minab, na baadhi ya watu na viongozi, muongo huu unapitia kati ya moshi na moto wa vita na uharibifu wa miundombinu uliofanywa na adui mwoga na shetani.

Alisisitiza kuwa muongo wa Karama mwaka huu ni mjumbe wa uthabiti na mapambano dhidi ya twaghuti kwa mfumo wa Hadhrat Ma‘suma (as), Maimamu, na Hadhrat Hujjah wa nane Ali bin Musa al-Ridha as, na akaongeza: Mwaka huu taifa letu chini ya uongozi na mwongozo wa Kiongozi wa tatu wa Mapinduzi, Ayatullah Hajj Sayyid Mujtaba Husseini Khamenei, (daamat barakatuh), linaendeleza njia ya Imam Khomeini Mkuu na Imam Khamenei shahidi; kwa sababu kuendeleza njia hii ni jukumu letu kubwa la Mwenyezi Mungu.

Muongo wa Karama mwaka huu ni wakati wa mazoezi ya kueneza matumaini na uthabiti mbele ya adui

Ayatullah Saeedi alisisitiza kuwa: Kuadhimisha kuzaliwa kwa Ahlul-Bayt (as) katika muongo wa Karama mwaka huu kunapaswa kuwa mjumbe wa ucha-Mungu, utii wa wilaya, na kulinda heshima na hijabu mbele ya mashambulizi ya kila upande ya maadui wetu waliolaani ambao kupitia uharibifu huu wanataka kutukatisha tamaa; hivyo basi, muongo huu unapaswa kuwa mazoezi ya kueneza matumaini na uthabiti mbele ya adui, kwa matumaini kuwa upinzani huu utaandaa mazingira ya utawala wa kimataifa wa Imaam Mahdi (ajtf) inshaAllah.

Kusiwepo na kusuasua kuhusu Mlango wa Hormuz

Imamu wa Ijumaa wa Qom aliendelea kwa kuashiria suala muhimu la kitaifa la Mlango wa Hormuz na kusema: Popote ambapo diplomasia ya mashambulizi ya Iran inapaswa kufafanua uwanja wa mchezo, haipaswi kusuasua; haipaswi Mlango wa Hormuz kubakia katika kiwango cha kukusanya tozo na mapato ya muda mfupi; bali ni moja ya sifa za kimkakati za Iran na chombo cha utawala katika anga ya kimataifa. Hivyo basi, nchi yoyote itakayoweka kanuni za kupita katika mlango huu, haitasimamia tu upitaji bali itaathiri mtazamo wa dunia, mahusiano ya kimataifa, mipangilio ya kiusalama na lugha ya mazungumzo na nchi nyingine.

Alisisitiza kuwa: Ima Iran itaweka kanuni za Mlango wa Hormuz au wengine wataweka; katika jambo hili muhimu hakuna nafasi ya pengo kubaki. Ikiwa hatutapanga uwanja, wengine wataupanga; ikiwa hatutakusanya, wengine wataunda muungano; na ikiwa hatutaweka mfumo, wengine watauweka.

Iran lazima ichukue hatua ya awali katika Mlango wa Hormuz

Ayatullah Saeedi akasema kuwa; Iran inapaswa kuchukua hatua ya awali katika Mlango wa Hormuz na wengine wachukue msimamo kuhusu mpango wa Iran, alisema: Hii ina maana ya kutoka katika hali ya kujibu tu na kuingia katika hali ya kuwa mbunifu, mtunga kanuni na mdai. Ikiwa Iran itasubiri wengine waseme nini na Uingereza na Ufaransa wafanye mikutano na kuwaalika India na China ili kuweka kanuni, itapoteza hatua ya awali.

Akielezea hatua zinazopaswa kuchukuliwa kuhusu Mlango wa Hormuz, alisema: Kwanza ni kuzialika nchi zote ambazo biashara yao inategemea njia hii ya maji; pili kuanza mashauriano na nchi za Kiarabu za eneo; na tatu kuelekea kuunda mfumo mpya kwa mhimili wa Iran katika nafasi ya kutangaza mfumo mpya wa usimamizi wa Mlango wa Hormuz.

Imamu wa Ijumaa wa Qom aliona umuhimu wa hatua hii si wa kidiplomasia tu, bali pia wa kiusalama, kimedia, kisiasa na kimkakati, na akaongeza: Ziara za wajumbe na uwepo hai wa Iran katika eneo, kuwaalika wadau wenye maslahi na kuwakusanya katika meza ambayo Iran imeandaa, ni dalili ya nguvu na uthabiti wa Iran. Diplomasia ya kujibu tu ni ya gharama kubwa, na ikiwa Iran itasuasua, kesho italazimika kucheza katika uwanja uliopangwa na wengine.

Vikosi vya kijeshi vya Iran ni nguzo kuu ya heshima na usalama wa kitaifa

Ayatullah Saeedi aliendelea kwa kuashiria tarehe 29 Farvardin, Siku ya Jeshi, na 12 Ordibehesht, Siku ya kuanzishwa kwa Sepah, akasema: Usimamizi wa Kiongozi shahidi wa Mapinduzi akiwa Amiri Jeshi Mkuu ulionesha kuwa vikosi vya kijeshi vya Iran ni nguzo kuu ya heshima na usalama wa taifa, na kuviimarisha si chaguo tu bali ni wajibu wa Qur’ani na ni sababu ya kuzuia maadui wababe kama Marekani na utawala wa Kizayuni. Sera hii imejengwa juu ya uelewa wa kweli wa vitisho, na siku ya Jeshi na Sepah ni fursa ya kurejesha ahadi kwa vikosi hivi vya kujitolea na mashujaa.

Akiashiria matusi ya Trump mhalifu dhidi ya Papa na kiongozi wa Wakatoliki duniani, alisema: Kwa kitendo hiki kila mtu alielewa kuwa Trump hafungamani na mantiki yoyote, na kusimama dhidi ya dhulma ni njia ya pamoja ya Manabii wote wa Mwenyezi Mungu.

Imamu wa Ijumaa wa Qom pia akirejea mikusanyiko ya watu mitaani alisema: Wa kwanza kupigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu na kuinua bendera alikuwa Hadhrat Ibrahim (as). Watu katika siku hizi kwa kupeperusha bendera ya Iran na Hizbullah shujaa katika mikusanyiko yao yenye malengo, wameifanya bendera hii kuwa bendera ya waliodhulumiwa duniani na kuwa sababu ya kuangusha bendera ya dhulma, ukafiri na ubeberu wa kimataifa. Na kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na kwa kuwakasirisha maadui, bendera hii ndiyo itakayoweka msingi wa kuinuliwa kwa bendera ya utawala wa kimataifa wa Mahdi (ajtf).

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha